Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jaji Jacobs Mwambegele ametoa wito kwa wazalishaji wa maudhui mtandaoni kuhakikisha taarifa zinazopandishwa katika kurasa zao zinasimamia weledi ili kuepuka uvunjifu wa amani nchi.
Ametoa wito huo wakati wa mkutano na wazalishaji wa maudhui mtandaoni uliofanyika leo Agosti 2025, katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam ambapo amewataka waandaji hao kuandika habari za kweli zinasosimamia sheria kanuni na maadili.
"Nawakumbusha juu ya umuhimu wa kuepuka matumizi mabaya ya akili unde ambayo inatumiwa na baadhi ya watu wenye nia ovu kusambaza habari za upotoshaji hasa kupitia mitandao ya kijamii," amesema.
Akifafanua zaidi amewataka kuzalisha maudhui yatakayo wahamisha wananchi kujitokeza katika kupiga kura kwakuwa ni haki yao kikatiba.
Ameongeza kuwa ni vema wazalishaji kutengeneza maudhui yatakayo wahamasisha vijana na watumiaji wa teknolojia kupitia mitandao ya kijamii kupata hamasa na kujitokeza kupiga kura katika uchaguzi unatarajiwa kufanyika mnamo Oktoba mwaka huu.
Awali akiwasilisha mada kuhusu maandalizi ya uchaguzi mkuu na ushiriki wa vyombo vya habari, Mkurugenzi wa Uchaguzi Ramadhan Kailima amesema Tume inatarajia vyombo vyahabari vitatumia kalamu zao na nyenzo walizonanzo kuhubiri amani katika kipindi chote cha mchakato wa uchaguzi.
"Tume imejiwekea utaratibu wa kuvishirikisha vyombo vya habari katika mchakato mzima wa uendeshaji wa uchaguzi huu ili kuweka uwazi na kuhakikisha wanashiriki kikamilifu, tunawaomba kutumia nafasi na fursa mlizonazo kuhakikisha kunakuwepo na taarifa za mara kwa mara za kuelezea kinachoendelea kuhusu uchaguzi, "Amesema Kailima
Mkutano huo uliwakutanisha Wazalishaji wa maudhui mtandaoni wakiwemo Bloggers, Youtubers na Wachoraji wa Katuni wenye kaulimbiu ya Kura Yako, Haki Yako, Jitokeze Kupiga Kura. habari vitatumia kalamu zao na nyenzo walizonanzo kuhubiri amani katika kipindi chote cha mchakato wa uchaguzi.
"Tume imejiwekea utaratibu wa kuvishirikisha vyombo vya habari katika mchakato mzima wa uendeshaji wa uchaguzi huu ili kuweka uwazi na kuhakikisha wanashiriki kikamilifu, tunawaomba kutumia nafasi na fursa mlizonazo kuhakikisha kunakuwepo na taarifa za mara kwa mara za kuelezea kinachoendelea kuhusu uchaguzi, "Amesema Kailima
Mkutano huo uliwakutanisha Waz
alishaji wa maudhui mtandaoni wakiwemo Bloggers, Youtubers na Wachoraji wa Katuni wenye kaulimbiu ya Kura Yako, Haki Yako, Jitokeze Kupiga Kura.
0 Comments