Mgombea Ubunge Jimbo la Kasulu Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Prof. JOYCE NDALICHAKO amewashukuru wananchi wa Jimbo hilo kwa kujitokeza siku ya kampeni za Dkt. Samia Suluhu Hassan mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM siku ya Sept. 13 Wilayani Kasulu.
Shukurani hizo amezitoa alipotembelea Soko la Sofya lililopo Kasulu Mjini na kuwapongeza wananchi kwa namna wanavyounga mkono juhudi za Serikali ya CCM kwa kufanya biashara na kujiongezea kipato na kuwahimiza kuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi CCM kwa Awamu nyingine.
Profesa Ndalichako ameelezea
mafanikio mbalimbali yaliyopatikana katika kipindi chake cha Ubunge 2020-2025
akitaja kuboreshwa kwa mazingira ya kibishara katika soko la Sofya, Mikopo kwa
wajasiriamlai, Ujenzi wa Shule mpya za msingi na sekondari pamoja na sekta ya
afya
Ametaja kuendelea kuimarika kwa miundombinu ya barabara mjini Kasulu huku akibainisha kuwa serikali mpya ya CCM itakapoingia madarakani imejipanga kufanya mambo makubwa Zaidi kwa wakazi wa jimbo la Kasulu mjini.
Aidha Prof. NDALICHAKO amewaomba
wananchi kujitokeza siku ya Uchaguzi kwa ajili ya kumpigia kura Dkt. Samia
Suluhu Hassan, Madiwani wote wa jimbo la Kasulu Mjini na Kasulu Vijijini Pamoja
na Jina La Joyce Ndalichako.
Profesa Ndalichako amekuwa Mbunge wa Kasulu mjini katika Kipindi cha 2020-2025 na awali alikuwa mbunge wa kuteuliwa kati ya Mwaka 2015-2020 na alishika nafasi za uwaziri wa elimu na Uwaziri wa Kazi kwa vipindi mbalimbali.
Jimbo la Kasulu Mjini ni miongoni mwa majimbo mawili yaliyopo katika wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma.
Kwa Mujibu wa Kanuni za tume huru ya taifa ya uchanguzi INEC Uchaguzi mkuu umepangwa kufanyika Octoba 29 mwaka 2025 kwa kuwachagua viongozi mbalimbali kuanzia Madiwani, Wabunge na Nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
0 Comments