Prof. Ndalichako afunika mji, achukua fomu Ubunge 2025

Mgombea ubunge katika jimbo la Kasulu Mjini Prof. Joyce Ndalichako amechukua Fomu ya kugombea Nafasi ya Ubunge katika jimbo la kasulu kwa awamu ya pili ya mhura wa uongozi katika jimbo hilo.

Zoezi hilo limefanyika Agosti 26 katika ofis ya msimamizi wa uchaguzi katika jimbo la Kasulu Mjini Ndg. Azizi katika ofisi za jengo la Halmashauri ya Mji Kasulu.

Viongozi wa CCM Kasulu wakishuhudia tukio la mgombea mteule wa chama hicho Prof. Ndalichaki akitia saini daftari la INEC


Aidha baada ya zoezi la Kuchukua Fomu za kugombea nafasi ya Ubunge katika jimbo la Kasulu Mjini Ndalichako alizungumza na umati uliojitokeza kumsindikiza katika zoezi hilo na kuwashukuru kwa kuendelea kumuunga mkono na chama cha Mapinduzi.

Ndalichako amewaomba wananchi kujitokeza katika zoezi la kampeni litakapofunguliwa rasim Agosti 28 ili kusikiliza Sera na kampeni za wagombea huku akiahidi kufanya kampeni za Amani Bila kutweza utu wa Mtu nawenye kuzingatia Demokrasi ya nchi na vyama vingine vya siasa.

Awali mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Kasulu Ndg. Mbelwa Abdallah amewashukuru wanachama wa Chama cha Mapinduzi kwa kuendelea kukiunga mkono Chama hicho katika Wilaya ya Kasulu huku akiwaomba wagombea wakafanye kazi ya wananchi.

Kwa mujibu wa mwenyekiti Mbelwa kampeni Wilaya ya kasulu zitazinduliwa Rasimi Agost 31 mwaka huu huku tarehe 28 na 29 ikiwa ni mipango ya uzinduzi wa kampeni Hizo


Post a Comment

0 Comments