Taasisi ya Kuzuia na
Kudhibiti Rushwa (TAKUKURU) imeiitaja Halmashauri ya wilaya Kibondo mkoani
Kigoma kufanya ubadhirifu wa fedha za usimamizi wa mitihani
Naibu Mkuu wa Taasisi ya
kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa Kigoma, Bw. John Mgallah alisema
hayo leo katika taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu utendaji na utekelezaji
wa mambo mbalimbali ya taasisi hiyo kwa kipindi cha Mwezi April hadi juni mwaka
huu ambapo jumla ya chambuzi za mifumo 15 zilifanyiwa kazi.
Bw. Mgallah amebainisha
kwenye taarifa hiyo kuwa Ubadhirifu huo ulifanyika kupitia katika malipo ya
posho ya mitihani ya darasa la saba yaliyotolewa kwa watu mbalimbali waliokuwa
wakisimamia mitihani hiyo ambapo malipo hayo yametajwa kutofuata mwongozo
Mgallah alisema kuwa
tuhuma hizo zinafuatia uchambuzi wa mifumo uliofanywa na taasisi hiyo ambapo
imebaini kuwa kulikuwepo na malipo ya posho kwa watumishi wa halmashauri hiyo
waliokuwa wakihusika na usimamizi wa mitihani hiyo ambapo malipo hayakuzingatia miongozo ya
fedha na maalipo kwa kazi hiyo.
Kutokana na matokeo ya
uchunguzi huo, TAKUKURU kupitia katika hatua ya awali wametoa ushauri kwa
uongozi na idara ya fedha ya halmashauri
hiyo kuzingatia sheria na miongozo ya
fedha ili jambo hilo lisijirudie.
Aidha imeelezwa kuwa baadaa
ya hatua shauri hilo linapelekwa idara ya uchunguzi ili kuchunguzi na kuchukua
hatua kwa wahusika kwa mujibu wa sharia za kudhibiti na kupambana na rushwa.
Akitoa maelezo kwa njia
ya simu kuhusiana na tuhuma hizo Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya
Kibondo, Diocles Rutema alisema kuwa bado hajapata taarifa hizo na kwamba
atakuwa tayari kutoa maelezo yake na ufafanuzi wa jambo hilo atakapopata
taarifa hiyo.
Taasisi ya kupambana na kudhibiti Rushwa TAKUKURU imekuwa na utaratibu wa kufanya ufuatiliaji wa kina wa shughuli za halmashauri zote ikiwemo kukagua uhalali wa matumizi iwa rasilimali za umma ikiwemo fedha za miradi na uwajibikazi wa watendaji.
0 Comments