Hospitali ya Rufaa Maweni – Kigoma kufanyikiwa upasuaji wa nyonga kwa mara ya kwanza


 Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni – Kigoma imeendelea kutoa huduma ya upasuaji kwa mgonjwa mwenye tatizo la nyonga ikiwa ni siku ya tano ya kambi ya matibabu ya kibingwa na Ubingwa Bobezi katika hospitali hiyo.

Akizungumza na waandhishi wa habari Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt Joseph Nangawe amesema wananchi hawanabudi kufika kupata huduma hiyo kwasababu wataalamu wanatoa huduma bora na ya umakini kwa wagonjwa.

“Hospitali na timu nzima ya upasuaji imefanya mandalizi ya kutosha kwanzia kuingia hospitali, hivyo niwahakikishie wananchi kuwa huduma hii ni salama lakini pia niendelevu na leo niupasuaji wa kwanza wa nyonga katika hospitali yetu” amesema Dkt Nangawe, Kaimu Mganga Mfawidhi.

Aidha Dkt Nangawe ameongeza kuwa Serikali imeendelea kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora kwa kuwapeleka madaktri Bingwa na Bobezi katika hospitali za kanda Pamoja na hospitali za rufaa ambao wanasaidia kutoa huduma kwa wananchi.

“Hizi ni jitihada za Serikali yetu ya awamu ya sita ambayo imekuwa ikileta madakitari Bingwa na Bobezi katika hospitali zetu za rufaa kwa lengo la kuwasaidia wangonjwa katika magonjwa mbalimbali hii ndiyo sababu ya hiki kinacho fanyika hapa leo” amesema Dkt Nangawe.


Baadhi ya madaktari wakielendelea na batibabu katika kambi ya Maweni mkoani kigoma

kwa upande wake Dkt Wilson Masanja ambaye ni Daktari Bingwa wa magonjwa ya mifupa kutoka Hospitali ya Kanda Bugando Mwanza amesema, katika kambi hiyo ya siku tano huduma ya kubadilishia nyonga kwa mgonjwa ambaye amesumbuliwa na tatizo hilo kwa muda mrefu imefanyika huku akitoa wito kwa wananchi kutumia Hospitali ya Maweni kupata huduma hizo.

“Mala nyingi huduma hizi ninapatikana katika hospitali kubwa za kanda lakini leo tumefanikiwa kufanya upasuaji huu mkubwa hapa, niupasuaji wa kwanza hapa Maweni hivyo wananchi wafike kupata huduma kwa sababu huduma hizi kuzifuata katika hospitali zinazotoa huduma hizi moja kwa moja ni gharam kubwa kuliko hapa” amesema Dkt Masanja.

Kwa mujibu wa Dkt Wilson Masanja ambaye ni Daktari Bingwa wa magonjwa ya mifupa kutoka Hospitali ya Kanda Bugando Mwanza amesema Upasuaji wa kubadilisha nyongwa kwa wangonjwa waliokuwa wanasumbuliwa na tatizo hilo kwa muda mrefu umefanyika katika hospitali ya Rufaa ya Maweni na umefanikiwa kwa asilimia 100.

Mwandishi. Halfani Rajabu

Post a Comment

0 Comments