Rais wa Burundi atangaza mkakati wa kila Mrundi anamiliki kiasi
cha Faranga MILIONI 1 ifikapo mwaka 2027kama sehemu ya mkakati wa chama tawala
nchini humo kuwezesha jamii kumiliki uchumi na kutokomeza umasikini wa kipato
Akihutubia katika mkoa wa Ngozi kwenye uzinduzi wa kampeni za
chama tawala kuwania kushika hatamu ya Udiwani na Ubunge katika uchaguzi
utakaofanyika june 5 mwaka huu, Rais Ndayishimiye amebainisha kuwa kupitia
kilimo cha mahindi, mpunga, mbogamboga na matunda umasikini utakoma na kila
mwananchi atakuwa na kipato.
Mheshimiwa Ndayishimiye amekiri kuwa kupitia misimamo ya chama
na maelekezo ya kitaalam kwa wananchi, Nchi ya Burundi imefanikiwa kukomesha
njaa na kwamba sasa ni kusaka pesa na kujenga makazi bora ili kila mwananchi
aepukane na kuishi kwenye nyumba za nyasi
Rais wa Burundi atangaza mkakati wa kila Mrundi anamiliki kiasi cha Faranga MILIONI 1 ifikapo mwaka 2027, amesema kupitia kilimo cha mahindi, mpunga, mbogamboga na matunda umasikini utakoma. Akiri njaa imekomeshwa sasa ni kusaka pesa na kujenga makazi bora @EveristeNdayishimiye pic.twitter.com/dA9GiXEUiT
— Prosper Laurent. Kwigize (Baraka) (@PeaceTanzania) May 13, 2025
Aidha Rais Ndayishimiye pia ametumia kampeni hizo kutangaza
mkakati wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kutangaza mpango wa kila
mwananchai kutumia gesi safi ya kupikia na kupunguza kiwango cha matumizi ya kuni
na mkaa kwa ajili ya upishi.
Ameeleza kuwa serikali ya Burundi Tayari imeweka mkakati madhubuti wa kusambaza gesi na kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala ili kupunguza au kukomesha uharibifu wa mazingira unaotokana na ukatazi wa miti kwa ajili ya kuni na mkaa
Katika hatua nyingine Raia wa Burundi wanaoishi nje ya bara la
afrika maarufu Diaspora wametangaziwa neema kufuatia Katibu mkuu wa chama cha
CNDD FDD Bw. Reveren Ndikuliyo pamoja na Rais Ndayishimiye kwa pamoja kutangaza
mpango wa kuwapa nafasia ya uanzishaji wa miradi ya kimkakati utakaorahishwa na
serikali ijayo itakayowapa ardhi bila kusumbuliwa na ametumia hotuba yake kutoa
maelekezo kwa idara inayohusika na uwekezaji kuwapa kipaumbele Diaspora
wanapoomba vibali na ardhi kwa ajili ya uwekezaji
Wakati huo huo chama tawala nchini Burundi kumejigamba
kufanikisha mkakati wa kuiunganisha Burundi na nchi ya Tanzania na DRC kupitia
katika mpango wa ujenzi wa Reli ya kisasa SGR ambayo ujenzi wake umeanza kutoka
Kigoma nchini Tanzania kwenda Bujumbura na Uvira kupitia mkoa wa Rutana na
Gitega
Katibu mkuu wa CNDD_FDD amesisitiza kuwa chini ya mpango huo wa
kuinua sekta ya usafirishaji, Jiji la Bujumbura litajengewa mfumo wa reli ya
kisasa kwa ajili ya usafiri na utalii katika jiji hilo kubwa la kibiashara
nchini Burundi
Burundi yajivunia mpango wa ujenzi wa Reli kutoka Tanzania hadi DRC, kuwrka miundombinu ya Reli katika jiji la Bujumbura. CNDD yatangaza mkakati wa kutumia Diaspora kukuza uchumi wa taifa. @R_Ndikuriyo ktk Kampeni #ToraNum1 pic.twitter.com/WP8ZUjveDG
— Prosper Laurent. Kwigize (Baraka) (@PeaceTanzania) May 13, 2025
Kampeni za Uchaguzi mkuu wa wabunge, na madiwani zinatangulia
miaka miwili kabla ya uchaguzi mkuu wa Rais utakaofanyika July 2027 kufuatia
mabadiliko yaliyofanywa katika katiba ya Burundi, ambapo awali chaguzi zote
zilifanyika kwa wakati mmoja
Prosper Kwigize
CA, Ngozi Burundi
0 Comments