Mbio za mwenge kuzindua miradi ya utekelezaji Kasulu mji

Halmashauri ya Mji Kasulu mkoani Kigoma, imejipanga kutekeleza uzinduzi wa miradi mbalimbali ya Serikali katika kampeni ya Mbio za Mwenge wa Taifa zinazotarajiwa kuanza itakapofika Septemba 2025 katika mkoa wa Kigoma.

Akizungumza na Buha Fm Radio leo mei 19, 2025 Baada Kikao cha maandalizi ya Mbio za Mwenge Mratibu wa Mbio Mwenge Ndg. Daudi Stinga amesema halmashauri ya Mji Kasulu imejipanga kufanya vizuri katika zoezi hilo ili kuendelea kushika nafasi ya kwanza kama ilivyokuwa mwaka 2024.

“Leo tulikuwa na kikao cha maadalizi ya mwenge kwa ajili ya halmashauri yetu ya Mji Kasulu mwaka jana tulifanya vizuri hivyo mwaka huu tunajipanga ili tufanye vizuri zaidi kuliko mwaka jana, Mkurugenzi amekuwa akitupa ushirikiano mzuri ndiyo maana leo tumekutana kujadili na kujipanga ili tufanye kwa ubora zaidi” Amesema Stinga.


Mratibu wa Mbio Mwenge halmashauri ya mji Kasulu Ndg. Daudi Stinga

Aidha Stinga amesema mwaka huu watazindua miradi mbalimbali ikiwemo miradi ya Afya, Elimu, Barabara, maji Pamoja na miradi ya mapato ya ndani huku akiwaomba wadau kuonga mkono jitihada za serikali katika kutekeleza miradi katika kukuza Uchumi wa nchi.

“Kwa mwaka huu tutaendelea kufuata vigezo kama ilivyokuwa mwaka jana tutazindua miradi ya afya,elimu, Barabara, miradi ya maji na miradi ya mapato ya ndani itakuwemo lengo kubwa tunaendelea kuangalia miongozo inasemaje na tunaimani wananchi wataendelea kutuunga mkono ili halmashauri yetu iendelee kufanya vizuri” Amesema Stinga.


                                Mratibu wa Mbio Mwenge halmashauri ya mji Kasulu Ndg. Daudi Stinga

Katika hatua nyingine Mwl. Zawadi Mnana ambaye ni mjumbe wa Mbio za Mwenge 2025 amesema mwaka huu wameanza mapema kujiandaa ili kubakia katika nafasi ya kwanza na nafasi za juu zaidi kitaifa.

“Kiukweli mwaka jana tulifanya vizuri lakini mwaka huu tumeanza mapema mandalizi ili kuhakikisha tunakuwa nafasi za juu zaidi kitaifa hivyo wananchi wajitokeze kwa wingi kama ilivyokuwa mwaka jana katika uwanja wa umoja” Amesema Mwl.Mnana.

Kwa upande wake Mwl. Michael Benezeth ambaye ni Mwenyekiti wa wakuu wa shule katika halmashauri ya Mji Kasulu amesema maandalizi yameanza mapema ili wajumbe wapate kupendekeza maeneo ambayo yanauhitaji ya kufikiwa na Mwenge wa kitaifa.


Wajumbe wa mkutano wa maandalizi wa mbio za mwenge kwa mwaka 2025 katika halmashauri ya mji Kasulu

“Kikao cha leo kilikuwa kizuri kwa sababu wajumbe wamepewa nafasi ya kuchagua na kupendekeza maeneo ya miradi ambayo mwenge utaangazia na kufikiwa, lakini pia kama tutachagua miradi mizuri iliyosimamiwa kwa ubora tutaweza kufanya vizuri na jambo la Mwenge ni la kitaifa hivyo kila mtu ni vizuri kushiriki” Amesema Mwl.Benezeth.

Halmashauri ya Mji Kasulu kwa mwaka 2024 katika zoezi la mbio za mwenge ilishika nafasi ya kwanza kati ya halmashauri nane za mkoa wa Kigoma na kushika nafasi ya 40 kitaifa hivyo mwaka huu wadau wa maendeleo ya mbio za mwenge wamejipanga kushika nafasi za juu zaidi kitaifa ili kuipa hadhi halimashauri na mkoa kwa ujumla.

Mwandishi na Picha. Sharfati Shinji

Post a Comment

0 Comments