Burundi yafanya uchaguzi wa wabunge kwa Amani

 

Maelfu ya raia wa Burundi wamejitokeza jana kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa Wabunge na Madiwani huku amani ikitawala katika vituo vyote vya kupigia kura na katika mitaa mbalimbali nchini humo. 

Buha News imezuru katika tarafa kadhaa za mkoa wa Burunga ambao awali ulitambulika kama Makamba, Tutana na Gitega ambayo ni makao makuu ya nchi na kushuhudia makundi makubwa ya wananchi wakipanga mstari kuelekea vyumba vya kupigia kura kwa amani.

Wakizungumza kabla na hata baada ya kupiga kura wananchai na viongozi wamekiri kuwa uchaguzi umeandaliwa vizuri na kwamba hakuna aliyekosa jina lake kwenye orodha ya wapiga kura na kwamba wana matumaini na uchaguzi ulio huru na haki

Mamia ya wapiga kura wakiwa katika kituo cha kupigia kura cha Sampeke wilayani Kayogoro alikozaliwa katibu mkuu wa CNDD-FDD kanali mstaafu Reverien Ndikuriyo

Je! Ni matarajio gani ya wananchi hususani katika mikoa ya pembezoni na vijijini baada ya kumalizika kwa uchaguzi huu, wengi wa wananchi wanakiri kuwa licha ya nchi hiyo kufanikiwa kushughulikia changamoto za ulinzi na usalama jitihada zinahitajika kwenye miundombinu. Mama huyu ni mmoja wa maelfu ya wanawake waliojjitokeza kutekeleza wajibu wao wa kikatiba

Bw. Sinzinkayo Sylvester ni mwangalizi wa ndani wa uchanguzi huo matika mkoa wa Makamba, kwa upande wake anaeleza kuridhishwa na taratibu zilizoandaliwa na Tume huru ya uchaguzi nchini Burundi CENI na kuweka bayana kuwa hana sshaka kwamba kila mwananchi mwenye sifa na aliyejiandikisha atapata haki yake

Katibu mkuu wa CNDD-FDD Reverien Ndikuriyo akiwasili katika kituo cha kupigia kura cha Sampeke wilayani Kayogoro mkoani Burunga, mapema jana ambapo alipiga kura yake katika kijiji alichozaliwa.

Katibu mkuu wa chama tawala cha CNDD-FDD Ndikiriyo Reverie ni mmoja wa wananchi waliojitokeza kupiga kura katika kituo cha shule ya msingi Sampeke iliyopo katika kijiji cha Nyantakara wilayani Kayogoro alikozaliwa, pamoja na kuridhishwa na mwamko wa wananchi kujitokeza kupiga kura anaamini kuwa chama chake kitashinda

Uchaguzi wa Madiwani na wabunge 2025 unatangulia uchaguzi wa Rais utakaofanyika mwaka 2027 kufuatia mabadiliko ya Katiba ya Burundi inayompa Rais kipindi cha miaka saba ya kuongoza tofauti ya miaka miwili ya wabunge na madiwani.


Hadi sasa amani imetawala nchini kote na wananchi wanaendelea na majukumu yao kama kawaida wakisubiri kutangazwa kwa matokeo rasmi ya nani kashinda ambayo yanatarajiwa kutangazwa na tume huru ya uchaguzi nchini Burundi CENI wakati wowote kuanzaia sasa.

Taarifa zisizo rasmi zinataja kuwa chama tawala cha CNDD-FDD kinaongoza katika matokeo ya awali na huenda kikapata ushindi wa zaidi ya 90% na hivyo kuwa na uhakika wa kuunda serikali.

Imeandikwa na. Prosper Kwigize

Bujumbura, Burundi

 

 

Post a Comment

0 Comments