Wafanyabiashara walia na kujaa kwa maji Ziwa Tanganyika

 

Wananchi na wafanyabiashara wa mwalo samaki wa kibirizi kata ya kibirizi mkoa wa kigoma wamelalamikia serikali baada ya maji kujaa katika ziwa Tanganyika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kuziba barabara jambo lilinalopelekea kushindwa kufanya shughuli zao.

Wamesema hayo leo kwa nyakati tofauli wakati wakizungumza na buha fm radio na kusema kuwa barabara hiyo ni takribani miaka miwili toka imevamiwa na maji ambapo maji hayo yamekuwa yakiathiri shughuli zao za kiuchumi.

“tumeshalalamika sana lakini bado changamoto hii inaendelea kuwepo sisi tunalipa ushuru wa manispaa wa maegesho kwa babaji n ahata ushuru wa soko lakini bado hatujajengewa eneo hili kwaiyo tunaomba serikali jambo hili linatuathiri sisi kiuchumi kulingana na shughuli zetu tunazofanya” wamesema wananchi wa kibirizi.


baadhi wa wasafiri wakisafiri kwa njia ya mtumbwi

Aidha wafanyabiashara hao wameongeza kuwa wamekuwa wakitumia gharama kubwa kusafirisha bidhaa zao kwa kutumia barabara inayotoka Soweto jambo linalowapa hasara katika biashara hizo.

“Kwanza tunapata athari kubwa kwa sababu hii njia haipiti usafiri wowote kulingana na maji yalivyojaa hapa inatulazimu kuzunguka na kulipia hela kubwa kwa sababu ya usafiri kukosekana na kuwa wa shida na wakati mwingine tunapata hasara sababu tunachelewa kufika sokoni kwa wakati” Amesema Asha Pitter moja wa wafanyabiashara.


Moja ya dereva bajaji katika kituo cha Kibirizi

Kwa upande wao madereva wa vyombo vya usafiri wanaotumia barabara hiyo wamesema kuwa abiria wamekuwa wakitumia mitumbwi kuvuka katika eneo hilo lakini pia hata kipato kimepungua kwa sababu wamekuwa wakizunguka sana ili kukwepa maji hayo.

“kwa sisi madereva abiria wetu wanapata shida sana kwa sababu wanavuka kwa mitumbwi hapa kwenda ng’ambo ya pili lakini pia hata kipato tunacho pata sasa hivi ni kidogo ukilinganisha na awali kuazia kwa boda na bajaji kwa ujumla” amesema moja ya madereva.

Mvua zinazoendela kunyesha katika mkoa wa kigoma zimeshababisha maji kuongezeka katika ziwa Tanganyika na kuingia katika maeneo ya shughuli za binadaamu pamoja na kuharibu makazi ya watu katika maeneo ya Katubuka, Kibirizi na Bangwe.

Mwandishi na Picha; Halfani Rajabu

 

Post a Comment

0 Comments