Mkuu wa Wilaya ya Karatu Dadi Kolimba amewataka Wakala wa barabara vijijini na mijini ( TARURA) Mkoa wa Arusha kutatua changamoto za Miundombinu kwa kuzingatia tahadhari ya mvua za El nino kuanza.
Akizungumza wakati akifungua kikao Kazi cha Watumishi wa Wakala wa barabara za mijini na vijijini Tarura kinachofanyika kwa siku mbili wilayani Karatu Mkoani Arusha, ambapo amesema taarifa za Mamlaka ya hali ya hewa nchini kuwepo kwa mvua hizo wanapaswa kujipanga kutatua changamoto kabla na baada ya mvua hizo.
Amesema Kuna shughuli ambazo zinatakiwa kufanyika kabla ya maafa lakini kunashughuli zinatakiwa kufanyika wakati wa maafa na Kuna shughuli ambazo zinatakiwa kufanyika baada ya maafa na miundombinu ni muhimu na keamba wahakikishe katika ile mipango yao inasimamiwa vizuri.
"Maeneo ambayo yamekuwa na changamoto mkayaweke vizuri kwa kuzibua mitaro kuweka makaravati kabla ya athari Kubwa haijatokea kwa kuhakikisha tunaisimamia vizuri ili mvua zinapokuja zisiwe na madhara makubwa"Alisema
Aidha amesema wote wana jukumu Kubwa la kuhakikisha barabara zote za vijijini na mijini zimekaa vizuri ili kusaidia kusitokee maafa makubwa kupitia kamati za wataalamu kuanzia ngazi za kata wilaya hadi Mkoa ,lakini pia endapo yatatokea maafa watahakikisha wanatumia vizuri Elimu zetu kuokoa ili kusije kukatokea maafa makubwa.
Kwa mujibu wa Kolimba Moja ya malengo yenu ni kujadili mipango ya huko mbeleni kwa sababu ya Utalii mjaribu kuimarisha miundo mbinu ya barabara zetu hapa mjini.
"Wakati Mimi naingia hapa 2021 tulipata bajeti ya million 928 lakini kwa mwaka wa fedha 2022/23 tumeanza kupata bajeti ya billion 2.3 ambapo wilaya ya Karatu Ina mtandao wa barabara kilometa 712 wakati naingia kulikuwa na barabara za lami km 0.6 Sasa kuna km 2.8."Alisema
Kwa upande wake kaimu Meneja wa Tarura Mkoa wa Arusha Mhandisi Albart Kyando amesema wamepokea maelekezo ya Mkuu wa Wilaya na wameshaanza kuchukuwa tahadhari zote kwa kuandaa Mpango mkakati kama taasisi wa kukabiliana na maafa kwa kufuata Muongozo uliotolewa na kamati ya maafa.
Hata hivyo amesema kwa Sasa wanakazi zilizofanyika na kwamba wamepokea tahadhari hizo tokea mwezi wa 7 na Kazi ya kwanza ilikuwa ni Madaraja na vivuko vyote ambapo baadhi ya changamoto wameshaanza kuchukuwa hatua kwa kutenga baadhi ya rasilimali ambazo zilikuwa watumie katika Kazi za kawaida hivyo itakapotokea wataendelea kukabiliana ili kupunguza athari.
"Mara nyingi bajeti zetu tumekuwa tunapanga kulingana na kufungua barabara mpya kutokana na vyanzo vya mfuko wa Jimbo na tozo kwa kipaumbele cha kwanza kuwa maeneo ya uzalishaji kwa kuongeza nguvu hivyo ni lazima tuwe na vipaumbele vya ujenzi ili kuondoa migogoro ambapo tumekuwa tukitoa Elimu kwa wananchi na madiwani "Alisema Mhandisi Kyando

0 Comments