Ampongeza Dkt. Biteko kwa kuweka msukumo wa Watumishi kuhamia Mtumba
Wizara ya Nishati
imepongezwa kwa kuhamia rasmi katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma
ambapo Idara na Vitengo vyote vya Wizara sasa vimeshahamia katika jengo la
Wizara lililopo katika Mji huo wa Serikali.
Pongezi hizo
zimetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu, Mhe. William Lukuvi wakati
alipotembelea jengo la Wizara katika Mji wa Serikali Mtumba ambapo alipokelewa
na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba, Naibu Katibu
Mkuu, Dkt. James Mataragio pamoja na Menejimenti ya Wizara.
"Nakupongeza
sana Katibu Mkuu kwa hatua hii, pamoja
na Mkandarasi wa Jengo na Msimamizi, pia
nawapongeza kwa nia thabiti ya kuhamia katika Mji huu wa Serikali baada ya Mhe.
Rais Samia kutoa fedha zilizowezesha ujenzi wa majengo haya Serikali
Mtumba". Amesema Mhe. Lukuvi
Ameongeza kuwa, nia ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa ufanisi katika eneo moja na hivyo kuondoa usumbufu wa kutumia muda mrefu kupata huduma katika maeneo tofauti.
‘ Nawashukuru
sana Wizara kwa kumheshimisha Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa sababu nia yake ni
Watumishi kuwa pamoja katika utoaji wa huduma ili kuleta ufanisi.” Amesema Mhe.
Lukuvi
Amempongeza
pia Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko kwa kuweka
msukumo kwa Wizara katika kukamilisha jengo hilo na kwa watumishi kuhamia
katika jengo husika.
Aidha Mhe.
Lukuvi ametoa rai kwa watumishi wa Wizara kuhakikisha wanatunza vyema
miundombinu na vifaa vilivyopo ili viweze kudumu kama ilivyokusudiwa.
0 Comments