Vyama vya siasa vyahimizwa kushiriki mchakato wa uchaguzi

Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 wa Halmashauri ya Mji Kasulu mkoani Kigoma Mwl. Vumilia Simbeye amewataka viongozi wa vyama vya siasa kuwa mstari wambele katika kuelimisha jamii kuhusu kujiandikisha na kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa unao tarajiwa kufanyika Novemba27,2024.

Wito huo aliutoa jana wakati wa kikao cha pamoja na viongozi wa vyama vya siasa kilichofanyika mjini Kasulu kwa lengo la kuhimiza ushiriki wa vyama vya siasa kwenye uchaguzi huo.

Mwl. Simbeye alieleza kuwa viongozi wa siasa bila kujali vyama vyao wanatakiwa kuwa mfano wa kuigwa na jamii kwakuwa wana wafuasi wengi ambao wanawatazama na kuwasikiliza 

Msimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa wa Halmashauri ya Mji Kasulu Mwl. Simbeye (aliyeketi mweye kofia) akiongoza kikao hicho

Amehimiza viongozi hao kutumia nafasi hiyo katika kusambaza elimu juu ya umuhimu wa kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kasulu Mbelwa Chidebwe akipokea vitendea kazi kutoka kwa msimamizi wa uchaguzi Mwalimu Vumilia Simbeye (kulia)  kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa.


Kwa upande wao viongozi kutoka CCM, CUF, ACT na CHADEMA wameahidi kutoa ushirikiano kwa kuhamasisha wafuasi wao kujiandikisha na kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa.

Hata hivyo wamehimiza kanuni za uchaguzi kuheshimiwa ili kuwa na uchaguzi huru na wahaki.

Akiongea kwa niaba ya wenzake Mwenyekiti wa CCM Bw. Mbelwa Abdallah amemhakikishia msimamizi wa uchaguzi kuwa vyama viko tayari kushirikiana na mamlaka za serikali za mitaa kufanikisha uchaguzi huo.

Wawakilishi kutoka CHADEMA na ACT Wakipokea vitendea kazi

Zoezi la uandikishaji kwenye daftari la orodha ya wapiga kura linatarajiwa kufanyika tarehe 11 hadi 20/10/2024.

Uchaguzi wa Serikali za mitaa uhusisha mitaa, vitongoji na vijiji na hufanyika kila baada ya miaka mitano na unasimamiwa na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI.

Mwandishi: Ellukaga Kyusa.

Mhariri: Prosper Kwigize.


Post a Comment

0 Comments